Tatizo ni lipi?

Usafirishaji haramu wa watu/biashara ya watu(Human Trafficking) ni nini?

Usafirishaji na biashara haramu ya watu (Human Trafficking) ni nini?
 
Usafirishaji na biashara haramu ya watu (human  trafficking) ni uhamisho wa mtu kutoka kwenye jumuiya yake na kwenda sehemu nyingine ndani  au nje ya nchi kwa ahadi za uongo, matokeo yake ni  kunyonywa kunyanyaswa, na kutumikishwa kwa kupindukia bila ya ujira kwa faida ya mtu mwengine, hii hujulikana kama utumwa mamboleo na ni moja ya matishio makubwa ya haki za binadamu. Ingawa usafirishaji na biashara haramu ya watu (human trafficking) huwatokea wanaume, wanawake na watoto, lakini inaonekana wanawake na watoto ndio wanaoathirika zaidi.

Usafirishaji na biashara haramu ya watu hutokea duniani kote na unyonyaji wa watu hutofautiana kati ya nchi na nchi (watoto kutoka Togo wanatumikishwa na kunyanyaswa katika mashamba ya kokoa Ghana, Wasichana wa Colombia wanalazimishwa ukahaba Japan n.k.)

Usafirishaji haramu wa watu/biashara ya watu katika Tanzania

Hali ya Usafirishaji na biashara haramu ya watu Tanzania.

Usafirishaji na biashara haramu ya watu (human trafficking) hutokea ndani ya Tanzania na kimataifa. Watu huletwa Tanzania kutoka Kenya, Uganda, Malawi na Burundi. Usafirishaji na biashara haramu ya watu unaoonekana kutapakaa sana ni ule wa ndani kwa ndani ya nchi unaolenga kuwanyonya watoto katika kazi za ndani.
Tanzania pia inatumiwa kama nchi ya kupitishia  wahanga wa usafirishaji na biashara haramu ya watu toka nchi za pembe ya Afrika(Ethiopia, Somalia) wanaopelekwa Afrika kusini: Kuna wimbi la wahamiaji haramu wanaoingia
Tanzania ambao serikali ya Tanzania inahisi miongoni mwao wapo wahanga wa usafirishaji na biashara haramu ya watu. Kuna ushahidi wa matukio ambayo yanaonyesha kuna wahanga wa usafirishaji na biashara haramu kutoka India na Pakistan kuletwa Tanzania.
 
Watoto wahanga wa usafirishaji na biashara haramu ya watu  waliosaidiwa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji/International Organization for Migration (IOM) wengi wao hutokea sana mikoa ya Iringa, Morogoro, Mbeya, Mwanza Singida na Dodoma. Zipo dalili kubwa kwamba Dar es Salaam na Zanzibar ndio vituo vikubwa wanaopelekwa wahanga hao. Watoto hao kawaida hutolewa vijijini kwa kuahidiwa maisha bora na elimu mjini na ndugu zao wa karibu au  watu wanaoaminiwa na wazazi wao. Wakati mwingine watoto hawa hutolewa na wazazi wao kwa ndugu kwa mategemeo watoto wao watapata maisha bora wakiwa mjini.
Lakini wakati mwingine hali huwa sio kama walivyotegemea. Unyonyaji ni pamoja na kumlazimisha muhanga kufanya ukahaba, kazi za ndani, biashara za mitaani, kuosha magari bila kupewa nafasi ya elimu na matibabu, bila chakula au chakula kidogo sana, kunyanyaswa kijinsia, kutukanwa, kupigwa, kutishwa na kufanyishwa kazi bila  ya ujira. Wengi wa watoto hawa wakifanikiwa kutoroka,  huishia mitaani.
 
Sababu
 
Elimu ni moja ya sababu kubwa. Upatikanaji mkubwa wa elimu mjini huvutia vijana wa kike na kiume kutoka vijijini, wahanga wengi waliosaidiwa na IOM ni watoto walioacha shule au  hawajawahi kwenda shule kabisa kijijini mwao (watoto wa kike 24 kati ya 34 waliosaidiwa mwaka 2007 hawakuwahi kwenda shule kabisa).
Kupoteza wazazi wote wawili. Hali hii husababisha watoto  kulazimika kutegemea walezi. 
 
Juhudi za serikali ya Tanzania
 
Mwezi wa Disemba katika mwaka 2000, Umoja wa Mataifa ulipitisha “Itifaki ya kuzuia, kutokomeza na kuadhibu usafirishaji na bishara haramu ya watu, hasa kwa wanawake na watoto”. Bunge la Tanzania liliridhia itifaki hii mnamo tarehe 24 mwezi Mei, mwaka 2006. Tayari Tanzania ilishapiga marufuku utumwa. Usafirishaji haramu wa watu/ biashara ya watu ni utumwa mamboleo.

Usafirishaji haramu wa watu/biashara ya watu katika Afrika Mashariki

Mwelekeo:

Tanzania:
Usafirishaji na biashara haramu ya watu ndani ya nchi (Aina itambulikanayo zaidi zaidi Tanzania):

  • Watoto na vijana wa kike na kiume usafirishwa katika biashara haramu kutoka vijijni kwenda mijini kwa ajili ya utumishi wa ndani ya nyumba.
  • Wasichana usafirishwa katika biashara haramu na kuletwa mjini na katika maeneo ya kitalii (Dar es Salaam, Arusha,  Zanzibar) na hulazimishwa kufanya ukabaha.
    Watu usafirishwa katika biashara haramu ya watu toka Bara kwenda Visiwani na kulazimishwa kufanya kazi kwenye ma baa na mahotelini. Pia kuna ripoti toka kwa maofisa toka Zanzibar kuwa baadhi ya wahanga hulazimishwa kufanya ukabaha.
  • Ripoti zingine toka kwa maofisa wa Zanzibar zinasema kuna usafirishaji haramu na biashara ya watu toka Bara kwenda Zanzibar kwa ajili watumishi wa nyumbani/ndani haswa kwa wasichana.
  • Usafirishaji haramu na biashara ya watu unaolenga vijana wadogo wa kiume kwa ajili ya kutumikishwa katika migodi na kazi za mashambani.
  • Ahadi za uhongo za kazi nzuri na elimu bora hutumika kama njia kuu ya kuwahadaa wahanga.

Usafirishaji na biashara haramu ya watu wa kimataifa

Zanzibar utumika kama njia ya mapitio ya wahanga toka Tanzania bara kuelekea Oman na nchi zingine za uarabuni kwa ajili ya kufanyishwa kazi za majumbani.(Ripoti toka kwa maafisa uhamiaji wa Zanzibar)

  •  Kuna ripoti zinazoonyesha kwamba kuna watanzania waliosafirishwa kwenda nchi za Afrika kusini na Ulaya.
  • Wahanga wa usafirishaji na biashara haramu ya watu huletwa Tanzania toka Kenya, Uganda, Malawi na Burundi, na kuna kuna matukio machache ya wahanga toka India na Pakistan.
  •  Tanzania pia hutumika kama mapitio ya wahanga wa usafirishaji huu toka Somalia na   Ethiopia kuelekea Afrika kusini (maafisa wa uhamiaji).

Taharifa za IOM:  Kufikia leo, zaidi ya wahanga 118 wa usafirishaji na uhamiaji haramu wa watu, wengi wao wakiwa watoto wa kike chini ya miaka 18 walioletwa Dar es Salaam kwa ajili ya kazi za ndani, pamoja na vijana wa kiume wamesaidiwa na IOM.
 

Kenya
  • Inaeleweka kama nchi ya kuanzia, kufikia na kupitia wahanga wa usafirishaji na biashara haramu ya watu na pia nchi ina usafirishaji na biashara haramu ya watu wa ndani kwa ndani ya nchi.

Usafirishaji na biashara haramu ya watu ndani ya nchi (Aina itambulikanayo zaidi Kenya):

  • Usafirishwaji wa biashara haramu ya watu toka vijijini na kuletwa maeneo ya mjini kama Nairobi na Mombasa kwa ajili ya kufanyishwa kazi za nyumbani/ndani na wengine kushurutishwa kufanya ukahaba.
  • Usafirishwaji wa watoto kwenye hii biashara haramu na kupelekwa kwenye fukwe za kitalii kwa ajili ya kushurutishwa kufanya ukahaba.
  • Wahanga wengi huwa wasichana na wanawake, lakini kwa kiasi kidogo pia vijana wa kiume pia wametambulika kama wahanga wa usafirishaji na biashara haramu ya watu.
  • Kuna ripoti za usafirishwaji wa watoto wa kiume kwa ajili ya kutumikishwa mashambani.

Usafirishaji na biashara haramu ya watu wa kimataifa:

  • Idara ya watotokatika wizara ya mambo ya ndani imeripoti karibuni kuhusu usafirishaji na biashara haramu ya watoto 30 wa Kenya kuletwa Tanzania kwa ajili ya kutumikishwa kwa kazi za nyumbani/ndani na mashambani.
  • Wahanga wa usafirishaji na biashara haramu wameripotiwa kusafirishwa kwenda nchi za Marekani, Afrika kusini, Tanzania, Denmark, Ujerumani, Italia na Uholanzi.
  • Wakenya haswa wasichana usafirishwa  (trafficked)kwenda nchi za Uarabuni kwa mara nyingi kwa ajili ya kufanyishwa kazi za nyumbani/ndani kupitia mashirika ya uongo ya kutafutia watu kazi.
  • IOM na UNHCR utuhumu wnawake wa kisomali wanaotafuta hifadhi za kisiasa, wana safirishwa katika biashara hii haramu ya watu kwenda Kenya kwa ajili kufanyishwa kazi za nyumbani.

Kenya pia utumiwa kama nchi ya pitio la wahanga wa usafirishaji na biashara haramu ya watu wanaotoka Ethiopia na Somalia kwenda Afrika kusini (Ofisa wahamiaji wa Kenya) na Asia kuelekea magharibi.

Taharifa za IOM: IOM inasaidia kupatikana kwa mswada wa Kitaifa wa hatua dhidi ya usafirishaji haramu na biashara ya watu (National Plan of Action again trafficking in Kenya), kwa kushirikiana na wizara za na asasi za kiraia. NPA intategemea kupitisha mwanzoni mwa mwaka 2007.

Uganda

Usafirishaji na biashara haramu ya watu ndani ya nchi:
Jeshi la Lord’s Resistance Army (LRA)
[1] limeripotiwa kuteka nyara watu wazima na watoto wa kiganda nan kuwatumia kama askari, wapishi, wabeba mizigo na watu watumiwao kuwaridhisha kinguvu kimapenzi wanajeshi. UNICEF inakisia kuwa zaidi ya watoto 12,000 wametekwa nyara kuanzia mwaka 2002.

  • Watoto wa kiganda pia wamekuwa wakisafirishwa katika hii biahsar haramu ya watu kwa ajili ya kunyonywa kwa kufanyishwa kazi na ukabaha. Familia masikini zimekuwa zikitowa watoto wao bila kujua kwa watu wanaowahamini baada ya kurubuniwa na matokeo yake watoto hawa ushurutishwa kufanya kazi kwenye mabaa, au kama makahaba wa barabarani au kufanya kazi kwenye mashamba ya kahawa na chai na kazi za ndani.
  • Jamii za wavuvi zimekuwa zikielezewa na NGOs kwamba ushiriki katika kunyonya watoto na kushiriki katika kufanikisha usafirishaji  wa biashara haramu ya watoto kuvuka mipaka ya nchi.

Usafirishaji na biashara haramu ya watu wa kimataifa:

  • Uchambuzi uliofanywa na watafiti wa IOM pamoja na uchambuzi toka kwa wasaidizi wa wahanga wa Uganda kati ya 2004–2007 unaelezea Uganda kama nchi inayotumika kutuma na kupokea wahanga pamoja na wasichana na wanawake husafirishwa toka Uganda kuelekea Ulaya (Uingeleza, Uturuki), vile vile wasichana na wanawake toka Asia ya kusini huletwa Uganda kwa ajili ya kushurutishwa kufanya ukahaba.
  • Ripoti toka kwa maafisa uhamiaji na polisi wa Uganda inalenga juu ya usafirishaji na biashar haramu ya wasichana toka India na nchi zingine za ki Asia ambao uletwa Uganda na kulazimishwa kufanya ukabaha.
  • Pia maafisa uhamiaji wa Uganda wameonyesha kuwa na wasi wasi kuhusu usalama wa waganda wanasafiri kwenda kufanya kazi katika nchi za mashariki ya kati, haswa Dubai.

Taharifa za IOM: IOM imefanikiwa kuwasaidia wanawake 115 na watoto wahanga wa usafirishaji na biashara haramu ya watu kurudi na kuungana na familia zao toka Uganda kwenda DRC.

Burundi

  • Ripoti za karibuni za wahandishi wa habari zinasema usafirishaji na biashara haramu ya watu ufanyika kwa wanawake na wasichana wa kirundi kwenda mashariki ya kati kama wafanyakazi wa ndani.
  • IOM iliweza kutambua baadhi ya matukio kiasi ya usafirishaji na biashara haramu wa watoto kwa ajili ya kutumikishwa kama wafanyakazi wa ndani au kufanya kazi kwenye mashamba.
  • Serikali ya Marekani inakisia kuna idadi ya watoto 7000 ambao walisafirishwa katika hii biashara haramu ya watu wakati wa mapigano ya kivita kwa ajili ya kufanywa askari.

 

Jinsi ya kumtambua mhanga wa usafirishaji haramu wa watu/biashara ya watu

 Mhanga anakuwa ana vigezo vitatu vifuatavyo kwa pamoja

1. Kuhamishwa kutoka katika jamii yake (Kigezo 1)
2. Kunyang’anywa uhuru wake (Kigezo cha 2)
3.Kunyonywa kwa njia ya kutumikishwa kwa kazi yeyote au kunyanyaswa (Kigezo cha
Huyu ni mhanga wa usafirishaji na biashara haramu ya watu.
 
Mhanga ni nani ?
 
 
Uhamishwaji:                        Upatikanaji, usafirishaji, uhamishwaj na mapokezi ya wahanga.               
Unyang’anyaji wa uhuru:    Vitisho au utumiaji wa nguvu au njia zingine za kushurutisha,  kuteka nyara/kutorosha mtu,udanganyifu,kuhadaa, kutumia vibaya madaraka, kuwekwa katika hali ya kuweza kudhuriwa au kupokea  malipo. au faida zingine ili kufanikisha kupata idhini kwa mtu kumtawala/kummiliki mtu mwingine.         
Sababu/Unyonywaji:           Kufaidika kifedha au faida zingine kupitia unyonyaji.

 
Vigezo vyote vitatu vinatakiwa viwepo na pia vinahusiana kati ya moja na nyingine kwa usafirishaji na biashara haramu ya watu kutokea
Isipokuwa: Kwa watoto shughuri na sababu tu zinatosha kuangalia kama ni wahanga.
 
Utajuaje?
Jiulize maswali yafuatayo
1)Je, mtu amehamishwa toka katika jamii yake kwasababu ameahidiwa au familia yake imeahidiwa
 kuboreshwa maisha yake au kalazimishwa kutoka katika jamii yake?               
NDIO / HAPANA
 
2) Je, huyo mtu ananyonywa na hawezi kutoka katika hali hiyo ya kunyonywa pindi akifika mwisho wa safari yake?
NDIO/HAPANA
Kama majibu yote ni NDIO, basi kitu kilichomtokea huyo mtu ni usafirishaji na biashar haramu ya watu.

YOU ARE VISITOR NO :

 
 
printemail