|
|
IOM
| |
IOM – taharifa na takwimu Upanukaji na ukuaji wa ujumla ndani ya shirika – Vigezo muhimu • Wanachama wameongezeka toka mataifa 67 mwaka 1998 mpaka mataifa 120 mwaka 2006 na inaendelea kuongezeka. • Matumizi kwa ujumla yameongezeka toka dola za kimarekani milioni 242.2 katika mwaka 1998 mpaka milioni 733.3 katika mwaka 2006, kiasi cha juu kilitumika mwaka 2005 ambacho ni dola za kimarekani $952 millioni. • Maeneo maalumu ya kazi (Field locations) ziliongezeka toka 119 katika mwaka 1998 mpaka zaidi ya 300 kwasasa. • Project hai ziliongezeka toka 686 katika mwaka 1998 mpaka zaidi ya 1600 mwaka 2006. • Wafanyakazi waendeshaji (Operational staff) waliongezeka toka kadilio la wafanyakazi 1,100 kati ya mwaka 1998 mpaka zaidi ya 5,400 kwasasa, wengi wao wakiwa kwenye maeneo maalumu ya kazi. Mfumo wa IOM umegatua zaidi madaraka, yaani umegawa madaraka kwenye vituo vyake mbalimbali badala ya kuwa chini na usimamizi na uongozi wa moja kwa moja mmoja. Mfumo wa IOM umebobea zaidi kwenye kutoa huduma. Kwasasa kuna misheni 16 Missions zenye kazi za kikanda /Regional functions (MRFs) ambazo zinafanya kazi kama vituo vya rasilimali. Mfuko kwa ujumla: Katika mwaka 2006, zaidi ya asilimia 96 ya mfuko wa IOM ilikua katika mfumo wa kujitolea katika miradi mbali mbali. Kibakiacho kina wakilisha bajeti ya utawala, ambayo utolewa na mataifa wanachama. Kiasi kidogo cha gharama za utawala: Ili kulipia gharama za moja kwa moja, IOM uwa inatoza asilimia 5 ya gharama za jumla ya mradi kwa ajili ya gharama za utawala. Gharama za utawala za IOM ni moja kati ya gharama za chini katika mashirika yote ya kimataifa. April 2007 * maeneo maalumu ya kazi hayamaanishi majengo ya ofisi za IOM pekee, bali hata pale ambapo wapo wafanyakazi wa IOM wakifanyaKatika mwaka 2006, zaidi ya asilimia 96 ya mfuko wa IOM ilikua katika mfumo wa kujitolea katika miradi mbali mbali. Kibakiacho kina wakilisha bajeti ya utawala, ambayo utolewa na mataifa wanachama. Ili kulipia gharama za moja kwa moja, IOM uwa inatoza asilimia 5 ya gharama za jumla ya mradi kwa ajili ya gharama za utawala. Gharama za utawala za IOM ni moja kati ya gharama za chini katika mashirika yote ya kimataifa. April 2007 * maeneo maalumu ya kazi hayamaanishi majengo ya ofisi za IOM pekee, bali hata pale ambapo wapo wafanyakazi wa IOM wakifanya |
IOM Tanzania |
Kutokana na uongezekanaji wa uwezekano wa kukumbwa na usarifishaji na biashara haramu ya binadamu (human trafficking) katika jamii ya watanzania, IOM ilipendekeza kuendeleza juhudi zake za kupambana na usafirishaji na biashara haramu ya binadamu. Tafiti zinaonyesha Tanzania inaanza kukabiliwa na tatizo la kuwa nchi ambayo unatumiwa kama njia ya kupitishia wahanga wa usafirishaji na biashara haramu ya binadamu, pia kama nchi wnayoletwa wahanga hata kama nchi inayotoa wahanga. Usafirishaji na biashara haramu ya binadamu Tanzania ufanyika zaidi ndani kwa ndani ya ndhi, vijana wa kike na kiume hutolewa toka vijijini na kuletwa mijini kwa ajili ya kufanyishwa kazi za majumbani , kazi za mashambani, uvuvi, migodini na ukahaba wa watoto. Katika ngazi ya kimataifa wanawake usafirishwa katika biashara hii haramu ya binadamu haswa kwa ajili ya ukahaba au kazi za majumbani. Shughuri zingine zihusikazo na uhamiaji zitakiwazo kuangaliwa ni pamoja na uthibiti wa HIV/UKIMWI katika jamii zisizo na makazi maalum; msaada wa kitaalamu katika menejimenti ya mipaka; ushirikiano katika jumuiya za nchi mabli mbali na uwezeshaji wa taratibu za uhamiaji katika jumuiya hizo; na uhamiaji wa maendeleo kwa kutilia maanani utumaji pesa nyumbani na kurudi kwa wazawa wenye ujuzi wa kitaalamu mbali mbali. Uhamishaji, Dharura na Menejimenti ya Uhamiaji Baada ya Migogoro
Wafadhiri
| Serikali ya Australia
| Serikali ya Canada
| Serikali ya Norway
| Serikali ya Marekani
| IOM Tanzania inasaidia kiasi cha wakimbizi kutoka Burundi 8,500 ambao wamekubaliwa kwenda kuishi nchi nyingine wanaishio kwenye kambi za wakimbizi Tanzania. Katika hii programu IOM inajihusisha na shughuri zifuatazo: Upimaji wa afya(Health Assessment): ikiwa pamoja na upimaji wa x-rays, vipimo vya mahabara, kuhakikisha wakimbizi hawasafiri na magonjwa ya kuambukiza/mlipuko. Upimaji wa kwanza ufanyika na kama kuna ulazima tiba pia utolewa. Upimaji na uangalizi wa afya kabla ya kusafiri nayo pia utolewa kabla ya wakimbizi hawajasafiri. Ufundishaji wa Utamaduni(Cultural Orientation): IOM utoa mafunzo ya utamaduni na utaratibu wa maisha ya wa nchi wanazokwenda wakimbizi kwa wakimbizi kuanzia miaka 15. mafunzo hutolewa kwa kutumia lugha inayoeleweka na wakimbizi kwa mfano kirundi. Mafunzo haya ulenga mambo muhimu ambayo mkimbizi atayakuta mwanzoni akifika nchi amayohamia. Safari: IOM kwa kutumia ndege za kukodi na za kawaida, huwasafirisha wakimbizi mpaka kituo chao za mwisho katika nchi wanayohamia. Miradi Mikubwa Uhamiaji wa wakimbizi wa kirundi kutoka Tanzania. Uhamiaji wa wakimbizi kwenda Canada Uhamiaji wa wakimbizi kwenda Australia Uhamiaji wa wakimbizi kwenda Marekani Uhamiaji na Afya Pamoja na kuwafanyia upimaji wa afya wakimbizi wanahamia nchi nyingine, IOM inatoka huduma za vipimo vya kifua kikuu kwa watu wanaofanya maombi ya visa za Uingereza kwa ajili ya kukaa kwa zaidi ya miaka sita. Programu hii ilianza mwaka 2005 baada ya IOM kupokea ombi toka kwa idara ya uhamiaji ya Uingereza mjini London(kwa kushirikiana na idara ya afya).
Uhamiaji Wafadhiri
| Imedhaminiwa kwa hisani ya mpango wa rais kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Idara ya Idadi ya Watu, Wakimbizi na Uhamiaji.(PRM)
| IOM inasaidiana na serikali ya Tanzania na jamii ya Tanzania kulivalia njuga suala la usafirishaji na biashara haramu ya binadamu (human trafficking) kwa kutoa msaada kwa wahanga wa usafirishaji na bishara haramu ya watu na kujenga uwezo kwa watoa huduma, wizara husika na mashirika yasiyo ya serikari katika kuwawezesha kukabiliana na mahitaji ya wahanga wa usafirishaji na biashara haramu ya binadamu. Hii program pia inatoa msaada wa muda mrefu na uhifadhi pamoja na kuisaidia serikali katika juhudi zake za kuzidisha uhamasishaji wa madhara ya usafirishaji na biashara haramu ya binadamu. Programu hii pia ufanyika Zanzibar na inajumuisha wizara zote za serikali ya muungano na serikali ya Zanzibar. Mradi Mkuu
Upigaji vita usafirishaji na biashara haramu ya binadamu kwa njia ya kuepusha, kuhifadhi na kusaidia wahanga |
Jinsi ya kuwasiliana na IOM |
IOM Tanzania Slipway Road, Off Chole Road, Plot No. 1365, Msasani Peninsula, Dar es Salaam, Tanzania P.O. Box 9270 |
| Tel: | +255 22 2602913 |
| Fax: | +255 22 2602782 |
| Email: | iomdar@iom.int |
| Name: | |
| International: | www.iom.int |
| |
| |
| |
|  |
|
|
| |
| print | email |
 |  | |

|