Uwe sauti yao

Jinsi ya kusaidia

Unga mkono juhudi za kupambana na usafirishaji na biashara haramu wa watu, kama unamjua mtu yeyote anaenyonywa na kunyanyaswa kwa njia hii ongea na viongozi jamii karibu na wewe, walimu, rafiki zako, familia kuhusu tatizo hili au hii tembelea tovuti hii www.uwe-sauti-yao.org

Unaweza kuleta mabadiliko !

Uwe sauti yao

Nia
IOM kuanzia mwisho wa mwaka 2005 imekuwa ikiendesha mradi wa “Ari ya kupambana na usafirishaji na biashara haramu ya watu” ( Counter trafficking initiative) nchiniTanzania kwa njia ya hatua za kukinga, kuzuia na kusidia wahanga, na imesaidia zaidi ya wahanga 100 mpaka sasa.
IOM inafanya kampeni ya kuhamasisha mwamko wa kupinga na kuelimisha jamii kuhusu usafirishaji na biashara haramu ya watu, kampeni ambayo imegharamikiwa na serikali ya Tanzania kupitia National Aids Control Program(NACP).

Kampeni hii inania ya kuamsha hisia za kuwahurumia wahanga na kujenga utashi wa kukemea na kutohalalisha watu wanaonyanyasa na kuwanyonya watoto na vijana.

Kampeni ya UWE SAUTI YAO italenga watu katika jamii yetu ambao wana sauti yakuweza kukemea usafirishaji na biashara haramu ya watu na ambao wanaweza kufanya mabadiriko katika jamii.
Ni mategemeo ya kampeni kuwahimiza watu waweze sema “Hapana, tabia hii hatu ruhusu ifanyike katika jamii yetu na kwa majirani wetu.” Kujisikia kuwa watu kuchukuliwa katika jamii yetu kwa nia ya kunyonywa na kunyanyaswa sio sahihi, na mimi ni lazima niseme wacha!

Vifaa/Nyenzo

IOM imefanya warsha mbali mbali juu ya upigaji vita usafirishaji na biashara haramu hapa Tanzania. November 20,21 na 22 IOM na Zayedesa (Zanzíbar Youth, Education, Environment Development Association) zilifanya warsha kwa ajili ya NGO mbalimbali na waandishi wa habari wa Zanzíbar kuhusu usafirishaji na biashara haramu ya watu. Warsha kama hiyo kwa waandishi wa habari itafanyika Dar es Salaam tarehe 5 Disemba. Vifaa/nyenzo zingine katika kampeni ni vipeperushi(brochures), picha kubwa(posters),stika(stickers) na kalenda za mezan zitasambazwa mikoani Tanzania Bara na Visiwani kupitia kwa NGO mbali mbali na asasi za kiraia.

Pia fulana na kofia za rangi ya njano pia zitasambazwa bara na visiwani kwa ajili ya kampeni ya UWE SAUTI YAO. Bonyeza kwenye picha za vifaa mbali mbali vinavyoonyeshwa hapo chini kwa kupata (download)picha kubwa.

Katika mwezi mzima wa Disemba, vipindi maalumu vya kampeni ya UWE SAUTI YAO, kampeni ya kuhamsha mwamko wa uwelewo wa usafirishaji na biashara haramu ya watu vitarushwa redioni,Clouds FM,east Africa radio and radio free africa na kwenye televisheni za ITV,EATV,chanel ten,TV, Star TV.

Kwa kusikia vipindi vya radio na kuona picha za television za kampeni bonyeza picha za video kwa TV na Audio kwa radio.

Downloads

PosterBrochureCalendar
 
StickerT-shirtCap
 
Audio1Audio2Audio3
 
 
Video1 Video2
 
 
Onyesho
 
 

Kutakuwa na onyesho kabambe katika ukumbi wa Amani katika hotel ya Blue Pearl iliyopo Ubungo Plaza siku ya tarehe 16 mwezi Disemba 2007. Onyesho hili ni moja kati ya juhudi za kampeni ya UWE SAUTI YAO ambalo litajumuisha wafanya maigizo maarufu Tanzania kina Muhogo Mchungu, Kipemba na wenzao, wanamuziki wa kizazi kipya kina Professor Jay, Banana Zorro, Enika na mwanamziki mashuhuri wa kwaya Frola Mbasha.

 

 
 
printemail